Kupuliza Mapovu
Nov. 16, 2012

Wanaastronomia wamepiga picha tukio adimu sana huko angani: liitwalo ‘kuzaliwa upya kwa planetary nebula’. Hili ni povu la gesi ndani ya povu la gesi lenye rangi ya kahawia, au nebula, kama unavyoweza kuliona katika picha hii. Nyota nyingi hugeuka nebula mwishoni mwa maisha yake, na wakati mwingine tukio hili hufanyika mara mbili kama ilivyo kwa hili.

Endapo nyota kama Jua letu inapomaliza mafuta yake yote, hutanuka katika umbo kubwa la red giant ambalo ni kubwa zaidi ya mara kumi ya saizi yake ya awali. Katika hali hiyo nyota huishiwa nguvu za kuweza kushikilia matabaka yake ya nje, ambayo huishia kutawanywa angani. Wakati huo huo mabaki baki ya kiini hushambulia matabaka hayo yaliyolegea kwa mionzi mikali sana kutoka ndani na kuyafanya yabadilike na kuwa planetary nebula – mawingu ya gesi yenye rangi rangi.

Mara chache sana huwa inatokea kiini pia hutanuka na kutengeneza nebula. Na ikitokea hivyo huwa tunasema ni ‘kuzaliwa upya kwa planetary nebula’. Ukilinganisha na maisha ya nyota nebulae (wingi wa neno nebula) huishi kwa mda mfupi sana. Hupotelea huko angani ndani ya miaka elfu tu! Hii husababisha ugumu katika kuziona nebulae na haswa zile zilizozaliwa upya. Lakini kwa wakati huu wanaastronomia wameweza kuipiga picha moja wapo.

Dokezo

Katika karne zilizopita, watu walikuwa wanafikiri wanaangalia sayari iliyozungukwa na gesi pale walipoona rangi rangi za planetary nebula kwa kutumia telescope na kusabisha kupewa jina hilo. 

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi