Kiwanda cha Kutengeneza Nyota Kinakufa
Nov. 6, 2012

Kwa kipindi kirefu sasa ulimwengu umekuwa ni kiwanda kikubwa cha kutengeneza nyota, umeshatengeneza nyota nyingi zisizohesabika kutokana na gesi na mavumbi yanayoelea angani. Ingawa kwa sasa kiwanda hiki kikubwa kinaonyesha kuanza kufa! 

Kutokana na kukusanya maada nyingi zilizozagaa, nyota changa zinaongezeka uzito- kama barafu inayobiringita kwenye theluji na baadae kuwa nyota kubwa sana. Wanaastonomia wamegundua kuwa hali hii haijitokezi kila mara. Ambapo kwa sasa nyota zinazaliwa chache sana, mara 30 ukilinganisha na dunia ilivyokuwa changa! Dalili inayoonyesha kwamba kiwanda kilichoshamiri cha nyota kimeanza kufa. 

Wanaastronomia wamefanya ugunduzi huu kwa kuchunguza uzalishwaji wa nyota kwenye galaxi ambazo zipo katika umbali tofauti tofauti. Kwa kawaida mwanga huchukua muda kusafiri na kufika kwenye uso wa Dunia, hivyo wakati tunaangalia galaxi za mbali, tunaziangalia kama jinsi zilivyokuwa zikionekana pale zilipotoa mwanga kwa mara ya kwanza - miaka bilioni iliyopita huko nyuma! Hii inamaanisha kuwa kwa kuangalia galaxi katika umbali tofauti tofauti, pia tunaangalia miaka tofauti toafauti. Wanaastronomia wanatumia telescope kama kifaa chenye nguvu cha kuangalia nyakati: wanaweza kuchukua picha za galaxi changa, wakati ni za muda mrefu sana. 

Wanaastronomia wanatabiri kuwa namba ya jumla ya nyota zote zinazozaliwa itaongezeka kidogo sana, na baada ya hapo uzalishaji utasimama moja kwa moja! Kutokana na hayo inaonyesha kuwa karibu nyota zote zimeshazaliwa katika ulimwengu. Kwa mfano Jua ndilo litatoa joto kwa ajili yako, watoto wako, wajukuu wako, vitukuu wako na vizazi vijavyo. 

Dokezo

Nyota hujizalisha; zinatengenezwa kutokana na mavumbi, lakini pia hulipuka na kutoa mavumbi zinapokufa. 

This Space Scoop is based on a Press Release from RAS .
RAS

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi