Nyota Kupe!
Dis. 7, 2011

Wanaastronomia wamepiga picha nzuri sana ya nyota ambayo imepoteza maada zake kutokana na nyota kupe!

Picha hii inaonyesha sehemu ambapo nyota kubwa (ina rangi nyekundu) na nyota kupe (yenye rangi ya blu) katika picha zilizopigwa katika tofauti ya mwezi mmoja na nusu, huku zikizungukana.

Viini vya nyota hizi mbili vinatenganishwa na umbali uliozidi kidogo sana wa ule uliopo kati ya Jua na Dunia. (Kwa kulinganisha, Jua na nyota yake ya karibu vinatenganishwa na umbali wa mara 870,000 ya umbali huu!). Kwa sababu nyota hizi zipo karibu karibu sana, nyota kupe imeshakula karibu nusu ya ujazo wa nyota kubwa.

“Tulijua kuwa nyota pacha hizi si za kawaida, na maada zinahama kutoka katika nyota moja kwenda nyingine,” anasema mwanaastronomia Henri Boffin. Lakini jinsi jambo hili linavyofanyika ni tofauti na vile wanaastronomia walivyokuwa wakitarajia.

Uvumbuzi mpya unaonyesha kuwa nyota kubwa ni ndogo kidogo ukilinganisha na wanaastronomia walivyofikiria hapo mwanzo. Hii inamaanisha kuwa haina ukubwa wa kutosha kujaza nafasi kati ya nyota mbili. Kwa ujumla, ina upana mkubwa wa kujaza robo ya umbali huu. Hii inafanya iwe vigumu kuelezea ni kwa jinsi gani maada zinapotea kuelekea katika nyota ndogo, kwani nyota kupe haiwezi kuifikia.

Wanaastronomia wanafikiri kuwa, kuliko kung’atwa na kupe, nyota kubwa imeamua kujitolea kutoa baadhi ya maada zake. Hivyo ile nyota ndogo hula kitu chochote kinachoingia katika njia yake kama kupe rafiki.

Dokezo

Baadhi ya nyota pacha humaliza mzunguko mmoja kuzungukana chini ya masaa 24, wakati nyingine huchukua maelfu ya miaka!

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi