Binamu Kipara wa Pluto
Nov. 21, 2012

Makemake ni sayari ndogo katika mfumo wetu wa Jua, inaonekana kukosa tabaka la hewa na kuifanya iitwe sayari kipara! Hii inamaanisha kuwa haina uwezo wa kuhifadhi mwanga mdogo wa jua inayoupokea katika umbali huo iliyokuwepo, ambao ni mrefu sana kutoka kwenye Jua ukilinganisha na sayari ndogo nyenzake ambayo ni Pluto. 

Ni katika siku za hivi karibuni ambapo sayari ya Pluto iliondolewa katika idadi ya zilizopo katika mfumo wa Jua. Ingawa sayari hii ndiyo iliyokuwa mbali zaidi kutoka kwenye Jua, na kwa sasa imejumuishwa katika kundi la sayari ndogo kama Makemake. Sayari ndogo kwa ujumla hazina sifa ya kuitwa sayari, ingawa bado zina sifa ya umbo la duara kama sayari na ni kubwa zaidi kuliko vimondo. Tunafahamu kidogo sana kuhusiana na sayari ndogo zilizo karibu yetu na hatujui chochote kuhusiana na sayari ya Makemake. Ili kuweza kuifahamu sayari hii, wanaastronomia iliwabidi waisubiri hadi iende mbele ya nyota. Basi wakaisubiri na baada ya muda subira yao ikazaa matunda.

Kama kungekuwa na tabaka la hewa linalozunguka Makemake, basi nyota ingefifia pale sayari hii ndogo ilipokinga mwanga wake. Mfano Jua linapochwea katika Dunia yetu, hufifia na kuzama katika kizio. Lakini kwa Makemake, sehemu ya nyuma yenye nyota hupotea ghafla na kutokea upya baada ya dakika moja, bila ya mwanga kufifia. Hii inatuambia kuwa Makemake haina tabaka la hewa na ina baridi kinyume na tulivyo itarajia, ambao ni zaidi ya ubaridi uliopo katika kizio cha kaskazini kwa wakati wa kipindi cha baridi!

Jifunze zaidi ni kwa vipi tabaka la hewa linaweza kuathiri jinsi sayari ya mbali inavyoweza kuonekana: buni kiumbe wako toka sayari ya mbali!

 

Dokezo

Zaidi ya Makemake kuna sayari ndogo nne zaidi zinazojulikana ndani ya mfumo wetu wa Jua: Pluto, Ceres, Haumea and Eris.

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi