Kuangalia Ndege Angani
Sep. 26, 2012

Je ushawahi kuangalia angani na kuona maumbo ya kufikirika yanayotengenezwa na mawingu? Wanaastronomia pia hufanya vitu vinavyofanana na hivyo, ijapokuwa mawingu wanayoyatumia wao yanaitwa nebula na yapo katika anga za mbali sana. Mawingu haya yanatofautiana na ale ya duniani kutokana na kutengenezwa na gesi na vumbi za angani, ukilinganisha na yale ya tunayo yaonayo angani yaliyotengenezwa kwa maji. Ambapo wanaanga wameweza kuona umbo linalofanana na kichwa cha ndege katika mzunguko wa wingu uitwao Seagull nebula.

Gesi na mavumbi ya angani ni vya baridi, hivyo having’ai na kutoa mwanga wa kutosha kuweza kuonekana kwa macho yetu, kwani vitu vyenye joto jingi ndivyo vyenye mwanga mwingi. Hali hii huweza kujitokeza katika hali ya kawaida pia, ambapo kama umeshawahi kushika balbu ambayo imewashwa kwa mda mrefu unaweza kuona kuwa ina joto sana! Na nebula katika picha unayoiona ni nyekundu kwa sababu ya nyota yenye joto kali iliyopo kati kati yake, nyota ambayo unaweza kuiona imekaa kama jicho la ndege seagull. Na joto kutoka katika nyota hiyo linafanya gesi zinazoizunguka ziweze kung’aa na kutoa mwanga unaoonekana.

Katika picha pia unaweza kuona ukungu wa rangi ya blu, je umeuona? Ukungu huu ni mavumbi ambayo yameangazwa na joto kutoka katika nyota changa zinazopatikana ndani ya nebula hii. Mwanga wa nyota hizo huakisiwa kutoka katika chembe chembe za mavumbi yapatikanayo angani na hivyo kuzifanya zionekane, kama vile unavyoweza kumulika kitu kwa tochi katika chumba chenye giza: ambapo utaweza kuviona vitu hivyo kwa sababu mwanga kutoka katika tochi yako huakisiwa na kurudi katika macho yako.

Picha hii inaonyesha sehemu ndogo tu ya nebula, ambapo wingu zima limetawanyika kama mabawa ya ndege katika sehemu kubwa ya anga na kufanya ionekane kama ndege anaruka angani! Angalia tena picha hii vizuri hapa 

Dokezo

Nyota inayoonekana katika kati ya picha hii (kwenye jicho la ndege) ipo pamoja na nyota nyingine ambayo ni jirani. Nyota hizi mbili zinazungukana na kufanya ziitwe nyota pacha “binary stars”! 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi