Sayari Ngeni Zinaweza Kuonekana Kama Maskani.
Okt. 4, 2017

Katika miaka ya 1980, chombo cha anga cha Galileo kiliipita Dunia kilipokuwa kinaelekea sayari ya Jupita. Kupita huku kulitupa nafasi ya kutumia vifaa madhubuti kuangalia dalili za uhai katika sayari yetu ya Dunia (Maskani). Dalili ambazo pia zingeweza kuonekana katika sayari nyingine zenye uhai. 

Wakati wakiiangalia Dunia, chombo cha Galileo kiliweza kuzitambua dalili zilizowazi za maisha. Maeneo yenye uoto wa nyasi na misitu yalikuwa yakisharabu miale ya mwanga ionekanayo kwa macho zaidi  (mwanga mweupe ambao macho yetu huweza kuuona ).Hii ni kwa sababu mimea husharabu mwanga na kuubadilisha kuwa nishati ili iweze kuishi.

Lakini kuna aina za mwanga ambazo mimea ya Dunia haiwezi kusharabu, kama Infrared (mwanga usioonekana kwa macho yetu). Hii ni kwa sababu mimea ya mwanzo Duniani ilikuwa ikimea chini ya maji. 

Maji ya bahari husharabu kwa haraka mwanga wa Infrared,wakati mwanga mweupe unaweza kupenya hadi kwenye kina cha bahari. Kwahiyo, mimea hii iliweza kuota na kukua kwa kutumia mwanga mweupe ulioweza kuifikia ndani ya maji – tabia ambayo bado ipo hadi leo.

Wakati wa kuangalia maisha katika sayari zingine,Wanasayansi mara nyingi huangalia nyota kibete (mbilikimo/ndogo) nyekundu, ambazo ndizo aina za nyota zilizo nyingi Ulimwenguni.

Nyota kibete nyekundu ni ndogo na zina jotoridi dogo kuliko Jua letu, na kiasi kingi cha mwanga zinazotoa ni Infrared. Hii imepelekea wanasayansi kuamini kwamba misitu na nyasi kwenye sayari zinazozizunguka nyota kibete nyekundu, zinasharabu mwanga wa Infrared zaidi kuliko mimea iliyo juu ya uso wa Dunia.

Hata hivyo, hii inaweza isiwe hivyo kama hii mimea mwanzo ilikuwa ikimea ndani ya maji, ambapo mwanga wa Infrared haufiki. Ilimradi kwamba inamea ndani ya maji ya bahari, mimea katika sayari nyingine inaweza kuonekana kama ile iliyopo katika Sayari ya Dunia.

Dokezo

Mimea ya mwanzo iliishi Duniani miaka bilioni 3 iliyopita. Hivi leo kuna aina zinazopata 400,000 za mimea zilizojitokeza toka katika mimea ya awali. Inatofautiana kwa vipimo kuanzia miche midogo hadi miti mirefu ya minara na mikubwa kuliko viumbe vingine.

This Space Scoop is based on a Press Release from NAOJ .
NAOJ

Gidion Kaweah / UNAWE Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi