Pendeza na Pinki
Mei 23, 2013

Chombo bora cha kuangalia Ulimwengu uonekanao kimetimiza miaka 15 leo. Happy Birthday Very Large Telescopes! Katika kusheherekea siku ya kuzaliwa telescope hiyo imetumika kupiga picha hii ya sherehe huko angani. Kauli mbiu ikiwa “Pretty in Pink” Pendeza na Pinki na kuna taa za disco na Maputo meusi yaliyosambaa katika picha. 

Ni kweli kuwa tunachokiangalia sio sherehe angani. Ingawa inaonekana kuwa na shamra shamra! Kitu haswa picha hii inayoonyesha ni wingu la kupendeza la gesi na vumbi ambalo wanaastronomia wanaliita ni stellar nursery. Hii ni kwa sababu ndani kabisa ya wingu hili la pinki, nyota mpya huzaliwa. Kwa bahati mbaya vumbi hilo jingi hunasa mwanga uonekanao kutoka katika nyota hizo mpya, hivyo telescope hii kubwa inashindwa kuziona. 

Ni nyota mpya zilizohifadhiwa katika wingu hili zinazofanya wingu hili ling’ae katika mwanga uonekanao. Mwanga wa nyota hizo hufanya vitu vilivyopo karibu kung’aa, na kupeleka nishati hiyo kwenye gesi na kuifanya ing’ae yenyewe. Kwanini ni ya Pinki? Kwa sababu maada mbali mbali hung’aa katika rangi tofauti tofauti. Wingu hili limetengenezwa kwa kiasi kikubwa na haidrojeni, kemikali inayopatikana kwa wingi sana katika Ulimwengu wote na haidrojeni hung’aa kwa rangi nyekundu au pinki. 

Likiwa limeambatana na mawingu meusi yanayoonekana kama Maputo: mlundikano mnene zaidi wa vumbi, ujulikanao kama Thackery’s globules. Makundi haya yametengenezwa katika maumbo ya ajabu kutokana na nguvu ya mionzi yenye moto itokayo katika nyota changa pembeni yake. Nguvu yake kubwa hubomoa mawingu haya na kuyasambaratisha, kama vile siagi inavyosambaratika ikiwekwa katika kikaango chenye moto. Kwa bahati mbaya kutokana na Thackery globules yatakuwa yameteketezwa hata kabla hayajafanikiwa kutengeneza nyota mpya.

 

Dokezo

Katika miaka yake 15 ya kutoa huduma Very Large Telescope imefanya uvumbuzi mkubwa! Hii ikijumuisha kuchukua picha ya sayari nje ya mfumo wa Jua ( ambayo unaweza kuiona kama tufe jekundu katika picha hii), kupima ukingo wa galaksi na mengine mengi! ( Na kama una shauku: imegundua kuwa Milky Way ina karibu miaka 13,600 bilioni. Itakuwa ngumu sana kupuliza mishumaa yote hiyo mara moja!)

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi