Ngome ya Galactic
Aprili 3, 2013

Galaksi yetu ya Milky Way ni zaidi ya mkusanyiko mkubwa wa nyota uliyojikunja, lakini pia ni kiini cha ngome kubwa inayotawala galaksi nyingine 20 ndogo zinazoizunguka. Kama ilivyo kwa Mwezi unavyoizunguka Dunia.  Nyota zinazowaka katika picha hii na michirizi ya gesi inayotoa mwanga katika picha ipo katika moja ya galaksi hizi ndogo iitwayo  Small Magellanic Cloud. 

Kama unaishi katika kizio cha kusini au karibu na mstari wa ikweta, unaweza kuwa umeona mawingu hafifu yenye ukungu katika anga lenye giza. Wingu dogo kati ya haya linaitwa Small Magellanic Cloud, moja ya satelaiti ya asili ya Milky Way galaksi. Ni galaksi ndogo, ikiwa inamaanisha kuwa ina nyota chache ukilinganisha na galaksi kama yetu. Ambapo galaksi yetu ina nyota karibu bilioni 300, yenyewe ikiwa na nyota zinazokaribia bilioni moja tu. 

Katika vipimo vya anga, galaksi hii ipo karibu sana na yetu ambayo inatembea katika mwendo kasi mkali mno ujulikanao ulimwenguni ( mwendo kasi wa mwanga) ambapo itatuchukua si chini ya miaka 200 kuifikia kutoka Duniani. Hii inaweza isionekane kuwa ipo karibu, lakini galaksi tuliyoizungumzia katika Space Scoop ya wiki Iliyopita itachukua miaka 47 ikiwa unasafiri katika mwendo kasi huo huo! 

Kwa galaksi hii kuwa karibu na sisi, kumewapatia wanaastronomia nafasi ya kuchunguza taarifa ambazo ni ngumu kuzipata kwa galaksi zilizo mbali zaidi. Katika picha linaonekana eneo lijulikanalo kama ‘Mabawa’, ambalo lina makundi matatu ya nyota ambayo wanaastronomia wamekuwa wakiyachunguza katika siku za karibuni ili kutambua ni kwa jinsi gani nyota huzaliwa. 

Dokezo

Wingu dogo la Small Magellanic Cloud lilianza kama galaxy ndogo ya kujiviringisha, kama ilivyokuwa kwa Milky Way galaksi. Baada ya muda galaksi ya jirani iliivuta na kuharibu umbo lake katika umbo lisiloeleweka tunaloliona leo.

This Space Scoop is based on a Press Release from Chandra X-ray Observatory .
Chandra X-ray Observatory

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi