Mabawa ya Seagull Nebula
Feb. 6, 2013

Nyota ing’aayo na michirizi ya nyota zinazowaka katika picha vinatengeneza Nebula nzuri ya Seagull. Umbo hili kubwa lililopo katika mfumo wa ndege limetengenezwa na mawingu matatu makubwa ya gesi: kichwa na mabawa mawili. Unaweza kuliona umbo lote kwa ukamili hapa. Pichani ni sehemu ndogo tu ya nebula yote. Je unaweza kukisia ni hiyo ni sehemu gani ya Nebula? Ni mabawa! Je ulipatia? 

Gesi nyekundu inayowaka katika picha sio tu kwamba inapendeza, bali pia ina taarifa muhimu. Rangi hiyo inawaambia wanaastronomia kuwa, hicho tunachokiangalia ni gesi ya hidrojeni – ambayo ni elementi inayopatika kwa wingi sana ulimwenguni.

Kuna maada nyingi sana hapa Duniani, ila ulijua kuwa kama ukizivunja vunja utatambua kuwa zimetengenezwa na chembe chembe za kikemikali chache muhimu? Tunaziita chembe chembe hizi ‘elementi’. Kwa mfano Carbon ni elementi, lakini ukiichanganya na elementi nyingine unaweza kutengeneza maelfu ya maada, kama vile sukari, plastiki na pombe. 

Tunaweza kuzipata chembe chembe hizi muhimu angani pia, kwa kuangalia rangi za mwanga tunaoukusanya. Ni nyota changa na zenye joto kali zilizotengenezwa ndani ya mawingu haya ambazo zinasababisha gesi ya haidrojeni kuwaka na kung’aa. 

Dokezo

Haidrojeni inawaka sana. Inawaka sana hadi ikawa inatumika kama mafuta ya vyombo vya kwenda angani roketi! Lakini hapo hapo, haidrojeni ndiyo inayowaka katika kiini cha nyota na kuzifanya zing’ae. Sasa ni nani anaishangaa? 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi