Anga ya Giza Yaonyesha Nyota za Kung’aa
Dis. 6, 2012

Katika hali ya kawaida, mwanga hutusaidia kuona. Lakini linapokuja suala la kuangalia anga la usiku, mwanga hutuzuia kuona. Taa za barabarani na zile za magari huathiri kuonekana kwa nyota, sayari na hata Milky Way, galaxi yetu. Unaweza kuona nyota 2500 kwa macho yako tu, lakini kama unaishi katika jiji kubwa au mji, nyota unazoziona ni karibu chini ya 10 katika mwanga wa kawaida! 

Picha hii ya kupendeza inayonyesha kundi la nyota lenye kung’aa likiwa pamoja na gesi zenye kuwaka waka katika Nebula ya Carina, ambayo ina kiasi kikubwa sana cha gesi, vumbi na nyota vilivyojichimbia katikati kabisa ya Milky Way. Kama unaishi katika kizio cha kusini cha dunia, basi unaweza kuona nebula hii katika wakati wa usiku hata bila ya kutumia msaada wa telescope. Lakini kama vilivyo vitu vingine vingi vya kushangaza vilivyokuwepo huko ulimwenguni, Carina nebula imetoweka katika upeo wa macho katika miji na majiji kutokana na uchafuzi wa mwanga (light pollution). 

Ni bahati kwetu kwani wanaastronomia wemetengeneza telescope yenye nguvu mno yenye uwezo wa kukuza, kuvuta na kupenya mabilioni ya kilometa ili kuweza kupiga picha hii. Picha ambayo imepigwa na telescope kubwa iliyopo katika jangwa la Chile, mbali kabisa na chanzo chochote cha mwanga wa barabarani. Imeweza kupiga picha hii ya kupendeza na yenye taarifa nyingi kuhusiana na Carina Nebula, nguzo zenye giza za vumbi zinazotawanya wingu la gesi linalowaka na makundi ya nyota zenye kung’aa. 

Dokezo

Katika Mwaka 2012, maelfu ya miji Duniani kote yalizima taa zote kwa muda wa lisaa limoja katika kusheherekea na kuhifadhi Dunia yetu. Hata wanaastronomia waliopo katika International Space Station (kituo cha kimataifa kinachoelea angani) pia walishiriki! Kama unataka kufanya anga letu la usiku kuwa jeusi na kufanya nyota zing’ae tembelea tovuti ya Dark Skies Awareness na uone ni kwa jinsi gani unaweza kusaidia! 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi