Sayari Pweke Iliyopotea Angani
Nov. 14, 2012

Sayari pweke imeonekana ikizubaa zubaa peke yake huko angani bila kuwepo kwa nyota inayoizunguka! Sayari hii yatima inafikiriwa kuwa ilitengenezwa katika njia ya kawaida kama ilivyo kwa sayari nyingine, kutokana na mabaki ya nyota changa. Kutokana na sababu fulani fulani nyota hii ilitoka katika eneo lake na kuishia kuzurura peke yake angani.

Sayari hazing’ai kwa kutoa mwanga wake zenyewe. Kama umeshawahi kuiangalia sayari ya Zuhura, Mars au Jupita angani wakati wa usiku, basi ulikuwa unaangalia mwanga wa Jua unaoakisiwa kutoka katika uso wa sayari hiyo. Kwavile sayari pweke hazipo karibu na nyota yeyote, basi haziakisi mwanga wowote na kuzifanya ziwe ngumu kuonekana. Wanaastronomia wanafikiria kuwa sayari hizi pweke zinaweza kuwa ni nyingi zaidi kuliko nyota katika galaxi yetu, ingawa tumekuwa na wakati mgumu kuziona! 

Imekuwa ni kazi ngumu kukokotoa ukubwa halisi wa vitu vilivyo mbali katika anga. Jaribu kuangalia boti katika usawa wa bahari au ziwa kisha jaribu kukadiria umbali wake na ukubwa wake! Ambapo inakuwa ngumu zaidi kuweka makadirio hayo iwapo kitu unachokiangalia ni cheusi sana na kinaelea angani. 

Wanaastronomia wamekubali kuwa wanaweza kuwa hawajakadiria sawa sawa ukubwa wa sayari hii ndogo – na inaweza kuwa hata sio sayari bali ni nyota iliyodumaa “brown dwarf”! Ambayo inafanana na nyota na ni kubwa zaidi kuliko sayari kwa kufikia ukubwa wa mara 80 zaidi ya sayari ya Jupita lakini bado ni ndogo sana kuitwa nyota. Nyota zilizodumaa huwa hazichomi mafuta yake ya hydrogeni katika kiini chake, kama nyota nyingine zinavyofanya na kufanya ziwe na jotoridi dogo la kuziwezesha kung’aa.

Haijalishi kama Dunia hii pweke ni sayari au la, bali usingetaka kuishi humo kwani; Kuelea katika usiku usio na mwisho katika anga, lazima kuifanye sehemu hii kuwa na giza totoro na pweke sana! 

Dokezo

Baadhi ya wanaastronomiwa wanasema kuwa kuna mara mbili ya idadi ya sayari hizi pweke ukilinganisha na nyota zilizopo katika galaxi yetu; wengine wanafikiri kuwa kuna idadi zaidi ya mara 100,000! 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi