Siri za Dunia ya Mbali
Okt. 11, 2012

Ndani ya Mwezi wa Kwanza mwaka 2005, chombo cha uchunguzi cha Huygens kilikuwa kikitatiza katika anga lenye ukungu la mwezi wa Titan, ambao ni mwezi mkubwa wa sayari ya Satani. Chombo hiki kilikuwa ni cha pekee na cha kwanza kutua katika sayari ya mbali kutoka Duniani, kitu ambacho si cha kushangaza ukizingatia kilichukuwa miaka 7 kufika huko! 

Titan ni moja kati ya sehemu zinazofanana na Dunia katika mfumo wa jua. Kama ilivyo kwa Dunia Titan ina tabaka la hewa, ingawa tabaka la hewa lake ni pana zaidi na limepanuka zaidi angani kuliko letu. Tabaka hili lenye ukungu linafunika uso wa Titan kwa rangi ya chungwa na kuuficha usionekane kwa macho yetu. Mpango wa Huygen’s ulikuwa ni kufichua siri hii ambayo leo tunaijua! Kupitia mamia ya picha zilizopigwa kutoka katika uso wa Titan

Hivi sasa ni karibu miaka 8 tangu tukio hilo lilipotokea, na bado wanasayansi wanazidi kuchunguza dunia hii ya ajabu kupitia chombo cha Huygen kama jicho lao. Ilichukua sekunde kumi za makashikashi tangu chombo hichi kilipoingia katika anga, kudunda kwenye ardhi, kuburuzika na hatimaye kusimama. Wanasayansi kukota katika European Space Agency wametengeneza modeli ya computa kuonyesha ni kwa jinsi gani kutua huku kuliweza kutokea.

Mda huu mfupi uliweza kuonyesha siri mpya kuhusu uso wa Titan. Kwa jinsi chombo hichi kilivyokuwa kinatembea wakati kilipotua, kilichonyesha tabaka jembamba la barafu katika uso wa Titan. Chini ya tabaka hilo ardhi ilikuwa kama mchanga ulio loa unaopatikana katika fukwe za hapa Duniani.

Dokezo

Titan ni mwezi wa pili kwa ukubwa katika mfumo wa jua, ni mkubwa zaidi ya mwezi wetu na ni mkubwa zaidi ya sayari Zebaki. 

This Space Scoop is based on a Press Release from ESA .
ESA

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi