Nyota Millioni 84 na bado tunazihesabu!
Okt. 24, 2012

Kamera ya astronomia iliyochukua picha hii mpya kutoka katika kati ya galaxi yetu imezifanya kamera zetu za digitali zionekane kama midoli ya kuchezea watoto.

Ukienda dukani kununua camera mpya, utaweza kusikia watu wanazungumzia kuhusu ukubwa wa kwa kutumia megapixel.  Megapixel hii hulingana na ubora wa picha zinazoweza kupigwa kwa kutumia kamera hiyo. Katika hali ya kawaida kamera za digitali huweza kupiga picha zenye ukubwa wa megapixel 10. Lakini kamera hii iliyotumika kupiga picha yetu hii maalum ambayo ilishikizwa katika telescope ilipiga picha hii ya kustaajabisha katika ukubwa wa megapixel 12,000!

Namba hiyo ya kushangaza haiishii hapo, kwani kutokana na picha hii yenye ubora wa hali ya juu, wanaastronomia wanaweza kuona zaidi ya vitu bilioni 173, ambavyo kati yake million 84 vimethibitishwa kuwa ni nyota! Na hii ni zaidi ya mara kumi ya idadi ya nyota ambazo wanaastronomia waliweza kuzichukua katika picha mbali mbali zilizowahi kupigwa kutoka kati kati ya galaxi yetu, iitwayo Njia Maziwa ‘Milky Way’.“

Kwa vile data hii mpya inatupa nyota zote kwa mkupuo, tunaweza kuhesabu nyota zote zipatikanazo katika sehemu hii ya Njia Maziwa,” anasema mwanaastronomia Dante Minniti. Wanaastronomia kupitia uchunguzi wa picha hii wameweza kufanya ugunduzi mkubwa sana ambapo walitambua kuwa kuna aina moja ya nyota iliyotawala zaidi, iitwayo ‘faint red dwarfs’, ambayo ni taarifa nzuri kwa wawinda sayari, kwani red dwarf stars hutumika sana katika kuchunguza dunia za mbali.

Jihusishe: Je ni kitu gani ungeweza kukigundua kama ungekuwa unashughulika na moja kati ya telescope kubwa zaidi Duniani? Papo hapo ili kusheherekea miaka 50 ya Kituo cha Anga cha Ulaya Kusini unaombwa kupiga kura juu ya kitu umbacho ungependa kichunguzwe na telescope yake kubwa iitwayo VLT! Bofya hapa kwa taarifa zaidi

Dokezo
None
This Space Scoop is based on a Press Release from ESO.
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha
Space Scoop Nyingine

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi

This website was produced by funding from the European Community's Horizon 2020 Programme under grant agreement n° 638653