Hadithi Angani
Mei 2, 2012

"Kioo, kioo katika ukuta, je ni nani amepauka zaidi?” Iliuliza nyota inang’aayo huku ikingalia taswira yake iliyoakisiwa katika punje za vumbi angani. Ilistaajabu sana iliposikia jibu. “Haya ni mawingu ya vumbi”

Sawa, ni kweli nyota haziwezi kuongea, lakini haya mawingu ya vumbi ni mazuri zaidi kuliko nyota zinazoyamulika. Yanaitwa nebula akisi (reflection nebulae) kwa sababu yana akisi mwanga kutoka katika nyota zilizo karibu nayo na nebulae ni neno la kilatini linalomaanisha ‘mawingu’

Nyota iliyoakisiwa imeonyeshwa katika rangi ya bluu na nyeupe katika picha. Vumbi pia hutengeneza mwanga wake wenyewe, mwanga ambao umeonyeshwa kwa rangi ya chungwa katika picha. Sehemu hizi zenye rangi ya chungwa zinaonyesha sehemu mavumbi yalipolundikana.

Macho yetu hayawezi kuona hata kidogo mwanga unaotoka katika vumbi, lakini darubini maalum iitwayo APEX inaweza kuona. Bila APEX, wanaanga badala ya kuona milundikano ya mavumbi wasingeona kitu chochote - pangekuwa na giza nene, ambalo lingezuia kutambua chochote kilichopo.

Lakini ni muhimu kwa wanaanga kuweza kutazama eneo hili, kwani nyota mpya zinazaliwa katika mawingu haya ya vumbi na gesi.

Dokezo

Darubini ya APEX inapatikana katika jangwa lililopo Marekani ya Kusini ambalo lipo mita 5100 juu ya usawa wa bahari!

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO

Mponda Malozo / UNAWE-Tanzania

Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi