Ni Zamu Yangu Kung’aa!
Aprili 25, 2012

Angalia picha hii ya kupendeza iliyosheheni nyota. Ni wapi jicho lako linapovutiwa katika picha hii? Je ni kwenye mkusanyiko wa nyota za bluu na nyeupe  zilizopo katikati upande wa kushoto? Huu ni mkusanyiko wa nyota changa, zenye joto kali.

Sasa bofya katika picha ili uone picha yote. Mkusanyiko wa nyota unaomeremeta bado upo pale pale (upande wa juu kushoto mwa picha), lakini kwa sasa kuna vitu vingi zaidi vinavyokupa shauku kuvitazama. Lakini wingu jekundu la gesi katika upande wa chini wa picha linaangaza zaidi na kukupa shauku kubwa ya kulitazama.

Pia mkusanyiko huo wa nyota upo karibu zaidi na wingu kubwa la gesi katika anga ya usiku, lijulikanalo kama “Eagle Nebula” (Tai Nebula) ambalo halijaonyeshwa katika picha. Lakini katika picha ambazo zinaonyesha  wingu hili kwa ukubwa zaidi, kundi nyota hilo hufifia na hatimaye hutoweka. Ooooh! Ni kwa kiasi gani limepoteza umaarufu!

Mara nyingi wanaanga (Astronomers) huwa wanapiga picha sehemu ndogo ya anga, hivyo vitu vingi hupuuzwa, kama kundi nyota hili ambalo linavutia kulitazama. Unaweza kujaribu mwenyewe: tumia mikono yako kufunika sehemu za picha hii ili kutengeneza picha nyingine tofauti. Je imekusaidia kutazama kitu ambacho hukukitambua kabla?

Dokezo

Hii ni picha mpya iliyotolewa na Kituo cha Kuangalia Anga cha Ulaya Kusini, pia wana picha nyingine nyingi unazoweza kuzipata kupitia: www.eso.org/public/images/archive/top100

This Space Scoop is based on a Press Release from ESO .
ESO
Picha
Chapisha

Bado una shauku? Jifunze zaidi...

Space Scoop ni nini?

Vumbua astronomia zaidi

Hamasisha kikazi kipya cha wavumbua anga

Marafiki wa Space Scoop

Wasiliana nasi